Tuesday, November 3, 2009

WADAU HII JE

                                                                  

Mwanaume mmoja nchini Zimbabwe ambaye alienda kwa mganga alirudi nyumbani kwake na kufanya mauaji ya kutisha ambayo polisi nchini Zimbabwe wanasema hayawajahi kutokea nchini humo.
Polisi walimtaja mwanaume huyo kuwa ni Elmon Mupombwa mwenye umri wa miaka 41.

Gazeti la serikali ya Zimbabwe la Sunday Mail lilisema kwamba Mupombwa aliwaua watoto wake watatu wenye umri wa miaka 11, 7 na 5 kwa kuwacharanga na shoka na pia aliwajeruhi vibaya sana watoto wake wengine wawili.

Mupombwa pia aliiua mifugo yake yote, ng'ombe watano, mbuzi 20 na kuku 17 na kisha alijinyonga mwenyewe.

Watoto wake wawili aliowajeruhi wamelazwa hospitali na hali zao ni mbaya sana.
Taarifa ya polisi ilisema kwamba Mupombwa alienda kwa mganga siku hiyo kabla ya kurudi na kuanza kufanya mauaji hayo.

Haikujulikana wazi aliambiwa nini na mganga huyo kiasi cha kuamua kufanya mauaji hayo.

Hali ngumu ya maisha nchini Zimbabwe inayotokana na kulega lega kwa siasa ya nchi hiyo, imesababisha kuongezeka kwa idadi ya watu wanaoenda kwa waganga kwa imani za kuondolewa matatizo yao na ugumu wa maisha

No comments: