Monday, September 14, 2009

HAYA NI MAAJABU.........

Kijana Calvino Inman, 15, hutirikwa na machozi mara tatu kila siku katika vipindi tofauti tofauti ambavyo hudumu kwa takribani lisaa limoja.

Ingawa Calvino anasema kwamba hahisi maumivu yoyote wakati machozi ya damu yanapomtiririka, wakati mwingine machozi hayo huyaunguza macho yake.

Kwa mara ya kwanza hali hiyo ilipomtokea mama yake anayeitwa Tammy Mynatt alipiga simu namba 911 kuita ambulansi.

"Kitu ambacho hunikatisha tamaa ni pale anaponiangalia wakati machozi ya damu yanapomtoka na kuniuliza 'Mama je mi ndio naelekea kufariki?" alisema mama wa mtoto huyo.

Lakini baada ya kuwaona wataalamu wengi wa macho na kufanyiwa vipimo mbalimbali kama vile MRI, catscan, na UltraSound bado sababu au tiba ya kutokwa na machozi ya damu haijajulikana.

Madaktari wote waliofuatwa walisema kwamba hii ndiyo mara yao ya kwanza kuona mtu akitokwa na machozi ya damu katika miaka yao yote ya udaktari.

Kinachomsikitisha mtoto huyo ni kitendo cha wanafunzi wenzake shuleni kumtania sana na kumuita 'Mnyonya damu'.



"Sihisi maumivu yoyote wakati machozi ya damu yanapotoka, inashangaza kuona damu ikitirika badala ya majimaji" alinukuliwa akisema Rashida.

No comments: