Friday, September 18, 2009

DUU KWELI MAMBO YANAZIDINA..


Tolu mpya wa dunia toka nchini Uturuki anatafuta mchumba baada ya kujizolea umaarufu duniani na kuingizwa kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness akihesabika kuwa ndiye mtu mrefu kuliko watu wote waliowahi kutokea katika historia ya dunia yetu hii.

Sultan Kosen mwenye umri wa miaka 26, amemwacha kwa mbali jamaa wa China aliyekuwa akishikilia taji hilo, Bao Xishun, ambaye ana urefu mita 2.36 tu.

Kosen ana viganja vikubwa vya mikono kuliko watu wote duniani. Viganja vyake vina ukubwa wa sentimeta 27.5. Miguu yake pia imevunja rekodi ya dunia kwa kuwa na ukubwa wa sentimeta 36.5.

Kosen alitambulishwa kwa dunia jana jiji London na amesema kuwa umaarufu mpya alioupata duniani utamwezesha kusafiri dunia nzima na kuweza kutengenezewa gari atakaloweza kuingia bila kujikunja kunja.



Sababu ya urefu wa Kosen ni kwamba alikuwa na tezi (uvimbe) kwenye mwili wake ambao uliharibu mfumo wa homoni zake za ukuaji na kumfanya aendelee kukua maisha yake yote, alifanyiwa operesheni na kuondolewa tezi hiyo mwaka jana na hivyo hatarefuka tena zaidi ya hapo.

Kosen alisema kuwa urefu wake ndio uliomsababishia apate tabu kupata mpenzi lakini anaamini kwa umaarufu alioupata sasa atapata mwandani wake. Wiki ijayo anaelekea Marekani kukutana na wachezaji wa mpira wa kikapu wa Marekani.

"Ndoto yangu kubwa ni kuweza kuoa na kupata watoto - natafuta mchumba" alisema Kosen.

No comments: