Friday, October 3, 2008

The Ngoma Africa Band ilifunika Frankfurt City



Si wengine bali ni The Ngoma Africa Band inayoongozwa na mwanamziki nyota Ebrahim makunja aka Ras Makunja "Bw.Kichwa Ngumu,kwa mara nyingine tena iliuhakikishia ulimwengu kuwa dansi lake la bongo ni moto wa kuotea mbali,
katika onyesho kubwa la aina yake la African and Caribbean Festival lililofanyika katika viwanja vya Robestock Park,ndani ya mji wa maghorofa marefu Frankfurt,Ujerumani,

Bendi hiyo hilifanikiwa kuwatia kiwewe washabiki wa mataifa mbali mbali kwa kutumia mdundo wake ambao wenyewe wanauhita Bongo Dansi,palikuwa na pata shika za nguo kuchanika pale wake kwa waume,watoto na wakubwa,vijana na wazee walipodatishwa
hakili na mziki huo wa ngoma africa band,mdundo huo wa nyimbo za kiswahili ulifanikiwa
kupenya mpaka katika madirisha ya majumba marefu ya mji huo na kuwatoa kijasho na kuwadatisha hakili washabiki !

Pia onyesho hilo la iana yake lilipata baraka ya wanahabari na wanahabari rasmi kutoka
Idhaa ya KISWAHILI ya Radio DEUTCHE WELLE wakiongozwa na Mtangazaji maharufu
Bi.SAUM MWASIMBA na wenziwe walikuwapo uwanjani kushudia mchaka mchaka huo
kati ya The Ngoma Africa na washabiki!

Pamoja ya kuwapo ulinzi wa kutosha hili watu lakini mziki wa Ngoma Africa uliweza
kuwatia kiwewe kuwanzia washabiki hadi walinzi(Body Guards),cha kufurahisha ni kuwa
mdundo huo haukumwacha mtu kwa tabia yao hiyo Ras Makunja na Kikosi chake ambacho kina wanamziki wachizani wa kucharaza vyombo hakina Chris-B,Said Vuai na
wengineo walifanikisha kazi hiliyokuwa ikisubiliwa na washabiki.
Hapo ijumaa 29-08-2008 Ngoma Africa watapiga Live katika onyesho lingine kubwa la
AFRIKA FESTIVAL,litakalo fanyika huko Altona, Hamburg,Ujerumani ambako nako wanasubiliwa kwa hamu na washabiki!

Jumamosi 30-08-2008 saa mbili na nusu usiku watapanda jukwaani katika onyesho lingine kubwa la wazi AFRIKA FEST litakalo fanyika katika mji KREFELD,nje kidogo ya mji wa
Koeln,ambako WATAVUNJA JUNGU,baada ya mwezi waRamadhani watakuwa wanategemea kupomoromosha nyimbo mpya kama kawaida yao,vitu hivyo vipya vitarekodiwa katika Studio(Bunge la mizengwe),Oldenburg.

Tunatarajia watatoka na nyimbo zenye vituko vipya.
Tuwatakie mafanikio mema wachizani wetu hawa Ras Makunja na Kikkosi chake The Ngoma Africa band.

3 comments:

Anonymous said...

Hizo ndizo zao vichaa wa The Ngoma Africa band tunawafahamu sana sana,
na mwenendo wao huo wa kuwadatisha hakili washabiki.

Anonymous said...

eh! bwana kaka braza Ras Makunja!
mbona kila kukicha unafungua ukurasa mpya na huo mziki wako?
unajua hapa Rocky Town,Mwanza.wenzio hatulali kwa hizi nyimbo zako kupitia Radio Free AFrica

Anonymous said...

Ras Makunja! Una gubu
kila siku vituko!vipi zogo lako na "Baba wa Kambo" mmehafikiana vipi?